NOTISI YA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA UTPC 2017

KUMB: Na. UTPC/ED/PC/046/17                                                      Agosti 01, 2017

Wenyeviti

Klabu za Waandishi wa Habari

Tanzania

 

Ndugu

YAH: NOTISI YA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA UTPC

Notisi hii inatolewa kwa mujibu wa kifungu namba 14 (viii) cha Katiba ya UTPC.

Mkutano Mkuu wa UTPC MGM utafanyika mjini Tanga tarehe 15 na16 Septemba 2017 katika ukumbi ambao utatangazwa baadaye.

AJENDA

 1. Kufungua Mkutano
 2. Kutangaza akidi ya Mkutano Mkuu
 3. Kupokea na kuthibitisha ajenda.
 4. Kupokea na kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu uliopita uliofanyika 7/10/2016
 5. Yatokanayo
 6. Kumchagua mjumbe mmoja wa Bodi ya Wakurugenzi
 7. Kuwachagua wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
 8. Kujadili na kupitisha mabadiliko madogo ya Katiba ya UTPC
 9. Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za mwaka 2016
 10. Taarifa ya utekelezaji kwa mwaka 2016.
 11. Taarifa ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2016
 12. Mengineyo
 13. Kufunga Mkutano

Iwapo kuna klabu ambayo inataka kupendekeza ajenda, ifanye hivyo ndani ya siku 7 tokea leo. Ajenda hiyo itumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC.

 

Abubakar Karsan

Mkurugenzi Mtendaji

Recommend to friends
 • gplus
 • pinterest