Mkutano Mkuu wa Dharura wa UTPC, wapitsha  Mpango Mkakati wa UTPC 2016 – 2020
wajumbe wa mkutano mkuu wa dharura wa utpc wa mwaka 2016
Wajumbe katika Mkutano Mkuu wa Dharura wa UTPC wa mwaka   2016

Mkutano Mkuu wa wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), umepitisha Mpango Mkakati wa UTPC 2016 – 2020 ambao umefanyiwa marekebisho na mfadhili Sida.

Mkutano huo ambao ulifanyika tarehe 6 na 7 Oktoba, jijini Mwanza, ulifunguliwa na Rais wa UTPC Bw. Deo Nsokolo ambaye katika hotuba yake  aliwaambia wajumbe kwamba UTPC imepata fedha kutoka kwa mfadhili Sida na kwamba sasa kazi zitaanza rasmi baada ya Mkutano Mkuu huu kumalizika.

Hata hivyo Rais aliwaambia wajumbe kwamba, katika Mpango Mkakati huu, UTPC itashughulikia suala la kuanzishwa kwa chama cha wafanyakazi cha kutetea maslahi ya waandishi wa habari.

Pamoja na mambo mengine wajumbe wa Mkutano Mkuu walipitisha maazimio kadha wa kadha ikiwemo mabadiliko ya katiba ya UTPC ambapo sasa UTPC itakuwa na Bodi ya Udhamini na mtaalamu wa masuala ya fedha ambaye ataingia kwenye Bodi ya Wakurugenzi.

Mbali na azimio hilo lakini pia wajumbe wa Mkutano Mkuu walijadili kuhusu muswada wa sheria ya habari na namna bora ya kufikisha maoni yao kabla ya muswada huo kupitishwa rasmi.

Katika majadiliano kuhusu kutoa maoni ya muswada wa sheria, wajumbe walikubaliana kuiomba Serikali kuongeza muda zaidi kwa waandishi wa habari kujadili na kutoa maoani juu ya Muswada wa Sheria ya Habari.

Lakini pia wajumbe wa mkutano mkuu walipitisha azimio la kuiagiza Bodi ya wakurugenzi ya UTPC kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya Mkutano utakao wakutanisha wanachama wa UTPC ili kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria ya habari.

Pia katika mkutano huo, taarifa za utekelezaji na ukaguzi wa hesabu za UTPC kwa mwaka 2015 zilipitishwa.

 

Matukio katika Picha

{phocagallery view=category|categoryid=20|limitstart=0|limitcount=0}

Recommend to friends
  • gplus
  • pinterest