• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Klabu sasa kuongozwa kwa uwazi

Tanga 1Viongozi wa klabu za waandishi wa habari (press clubs) toka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani, wameahidi kubadilika na kuziongoza klabu zao kwa uwazi, ushirikiano na ufanisi wa hali ya juu.

Msimamo huo ulitolewa na viongozi 26 wa klabu hizo, waliokuwa kwenye mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, yaliyofanyika Tanga wiki iliyopita.

Mafunzo hayo yaliyotolewa na UTPC, katika mkakati wake wa kuwajengea uwezo viongozi wa klabu hizo.

Mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ni historia ya migogoro kwenye klabu, mikakati ya usuluhishi wa migogoro, sifa za uongozi na maana ya uongozi.

Mada nyingine zilizotolewa ni mgawanyo wa majukumu baina ya viongozi, sifa za sekretarieti inayotekeleza wajibu wake vizuri na zingine ni namna ya kuitisha na kuendesha vikao na mikutano ya klabu, mfumo wa udhibiti mapato na matumizi na nyaraka mbalimbali za mapato na matumizi.

Washiriki walifurahishwa sana na mafunzo hayo, na walielezea utayarifu wao wa kuyatumia kwenye kusimamia klabu zao.

Hatahivyo walielezea migogoro kwenye klabu na ujuzi mdogo kwenye utafutaji fedha, kama changamoto kubwa zinazokabili klabu zao.

Awali, akifungua mafunzo hayo, Makamu Rais wa UTPC, Bibi Jane Mihanji, aliwarai viongozi hao, waziongoze klabu zao kwa uwazi na ufanisi.

Mafunzo hayo tayari yamefanyika katika kanda za Ziwa, Magharibi, Kaskazini na Mashariki.

Kanda ambazo mafunzo haya hayajafanyika ni kanda za Kati, Kusini na Nyanda za juu Kusini na Zanzibar.

Unweza pata picha zaidi hapa

Mkurugenzi Mten...
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan, akiongea na washiriki Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan, akiongea na washiriki
Makamu Rais wa ...
Makamu Rais wa UTPC, Bi Jane Mihanji akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo. Makamu Rais wa UTPC, Bi Jane Mihanji akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo.
Baadhi ya washi...
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa klabu wakifuatilia kwa makini mafunzo Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa klabu wakifuatilia kwa makini mafunzo
Baadhi ya washi...
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, wakifuatilia kwa makini mafunzo yanavyoenda. Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, wakifuatilia kwa makini mafunzo yanavyoenda.
Baadhi ya washi...
Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, wakifuatilia kwa makini mafunzo yanavyoenda. Baadhi ya washiriki wa warsha ya mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, wakifuatilia kwa makini mafunzo yanavyoenda.
Viongozi wa Mor...
Viongozi wa Morogoro Press Club wakijadiliana katika kikundi Viongozi wa Morogoro Press Club wakijadiliana katika kikundi
Viongozi wa Dar...
Viongozi wa Dar City Press Club wakijadiliana katika kikundi Viongozi wa Dar City Press Club wakijadiliana katika kikundi
Viongozi wa kla...
Viongozi wa klabu za Dar, Morogoro na Pwani na maofisa wa UTPC katika picha ya pamoja, mara baada ya kumaliza mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, yaliyofanyika Nyumbani Hotel, Tanga wiki iliyopita Viongozi wa klabu za Dar, Morogoro na Pwani na maofisa wa UTPC katika picha ya pamoja, mara baada ya kumaliza mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha, yaliyofanyika Nyumbani Hotel, Tanga wiki iliyopita

 

News Archive

Our Videos

video