• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Taarifa kwa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida juu ya waandishi kufanyiwa vurugu wakiwa kazini na kunyang’anywa vitendea kazi vyao na polisi

policeNOVEMBA 22, 2013 Mimi Emmanuel  Michael  wa Star  TV/ RFA na mwenzangu  Leonard Manga wa TBC na  Hillary Shoo wa Gazeti la Jamboleo tuliombwa kuongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro  Nyalandu katika ziara yake katika katika eneo la Msitu wa asili wa Mgori ambako kuna zoezi la kuwaondoa kwa nguvu wananchi waliovamia  hifadhi hiyo.
Mhe Nyalandu  ambaye  pia ni mbunge wa eneo hilo alilazimika kwenda kwenye hifadhi hiyo baada ya kuwepo malalamiko ya wananchi kuchomewa nyumba zaidi ya 70 bila kuruhusiwa kutoa vyakula na mahitaji mengine muhimu, kupingwa na kufanyiwa vitendo vingine vya ukikwaji haki za binadamu.
Baada ya kufika huko wakati  Naibu Waziri  akiendelea kuzungumza na viongozi  kupata taarifa, sisi tulianza  kupiga picha za nyumba zilizochomwa na kufanya mahojiano na wananchi kisha kwenda kwenye eneo la mkutano.
Tukiwa kwenye  eneo la mkutano huo kumsubiri Naibu  Waziri  aje kuhutubia, askari  zaidi ya 20 wakiwa na magari manne walifika na kutuvamia kisha kutukwida na kutunyang’anya kwa nguvu kamera, Notebook na simu  kwa madai ya kuingia kwenye msitu huo na kupiga picha bila kibali.
Dakika chache baada ya Naibu Waziri kufika na kuongea na viongozi wa askari hao  kuwasihi waturejeshee Kamera na Note book ili tufanyie kazi lakini waliendea kugoma kwa zaidi ya saa tatu tangu saa tano  hadi saa nane mchana.
Baada ya Mazungumzo ya muda mrefu  hatimaye  polisi  hao walikubali  kurejesha Kamera lakini  zikiwa hazina  kadi yaani Memory Cards za kurekodia hivyo kushindwa kuendelea kufanyakazi.
Hali hiyo ilimfanya Mhe Nyalandu  kuzungumza tena na viongozi wa askari hao zaidi ya  mara tatu ndipo  walipokukubali kurejesha kwa masharti ya kurejesha kukaguliwa  tena baada ya kumaliza mkutano.
Hata hivyo licha ya  kupata kadi hizo baadhi ya picha katika  kadi hizo zilikuwazimefutwa na kadi moja ya Kamera ya mwandishi wa TBC haijapatikana  wala kurejeshwa hadi hivi sasa zaidi ya  askari kutupiana mpira.
Naibu Waziri Nyalandu amelaani kitendo hicho na kuahidi kuzungumza na viongozi wa juu wa jeshi la polisi.
Maoni
Mimi binafsi nimesikitishwa sana na kitendo cha Polisi kutufanyia vurugu, unyanyasaji na kutunyang’anya vitendeakazi vyetu suala ambalo linakiuka msingi ya Uhuru wa kupashana habari.
Pamoja na kubaki  na uamuzi wangu binafsi kama mwana  habari niliyetendewa kitendo hicho tena mbele ya  mmoja wa viongozi wa juu Serikali, naomba Klabu ichukue hatua dhidi ya suala hilo kwa mustakabali wa Uhuru wa habari  nchini.
Ikumbukwe kuwa  askari polisi waliotuvamia na kutufanyia vurugu walikuwa  na silaha za moto hivyo chochote kingeweza kutokea.
“ Nionavyo  mimi uandishi wa habari unaendea kuwa moja ya taaluma zinazohatarisha  sana maisha,  na huu ndio ujumbe pekee kwa wanahabari wenzangu”

 

News Archive

Our Videos

video