• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

MAENDELEO YA MRADI WA KAGERA PRESS CLUB ULIOFADHILIWA NA TMF

kageramapUTPC ilingia mkataba na Tanzania Media Fund (TMF) kusimamia mradi wa uchunguzi wa Uzagaaji wa silaha za moto Mkoani Kagera, unaotekelezwa na Club ya Waandishi wa Habari Mkoani Humo .

Mradi huo wa miezi sita ulianza rasmi tarehe 1/10/2013 na unatarajiwa kukamilika tarehe 31/03/2014. Katika hatua ya kwanza ya Mradi huu  jumla ya wanachama 15 kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Kagera walipatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa muda wa siku nne .

 Katika hao 15 , 6 walichaguliwa kwa ajili ya kutekeleza mradi husika na kutiliana saini  na UTPC .

Mbali na mafunzo hayo Klabu ya Waandishi wa Kagera ilipatiwa vifaa kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa mradi huo. Vifaa hivyo ni  Kompyuta mpakato 2, Kompyuta ya mezani (desktop) 1, vinasia sauti vya kisasa 5, Kamera 3.

Katika hatua ya kwanza matokeo ya awali yaliyopatikana  ni pamoja na watu kuingia nchini kiholela, kugundulika kwa viwanda vya utengenezaji wa silaha za jadi (Ngobole), mauaji, utekaji nyara na wizi wa kutumia silaha.

Kwa sasa mradi uo uko katika hatua ya pili ya utafiti ambayo inatarajiwa kukamilika tarehe  28/02 /2014.

News Archive

Our Videos

video