• Font size:
 • Decrease
 • Reset
 • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Wadau wa vyombo vya habari Tanzania waazimia kuisaidia tasnia ya habari

wadau

Pichani ni wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa waliohudhuria maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe 3 mwezi Mei.

Mwaka 2015, maadhimisho haya yamefanyika kitaifa mkoani Morogoro kuanzia tarehe 2 hadi 3 mwezi wa Mei.

Maadhimisho haya ya siku mbili, yalitangulia na shughuli mbalimbali zikiwemo uwasilishaji wa mada mbalimbali.

Mada hizo ni pamoja na “Better Reporting and Independent Journalism in the Digital Age, iliyowasilishwa na Erick Wambura (Senior Journalist and Correspondent for the East African) “Gender and Media” iliyowasilishwa na Valerie Msoka (TAMWA Executive Director) “Towards Better Digital Safety for Journalists and Their Sources” iliyowasilishwa na Maxence Melo (Jamii Forum CEO)

Hata hivyo, waandishi wa habari wakongwe walipewa muda wa kuelezea uzoefu wao wa kazi katika tasnia ya habari. Veterans waliopata nafasi hiyo ni pamoja na Masoud Masoud, Hamza Kasongo, Pili Mtambalike, Pascal Mayala, Ndimara Tegambwage na Eda Sanga.

Siku ya kwanza ilihitimishwa kwa waandishi kutoa shuhuda mbalimbali kuhusu Media Freedom Violations ambapo Maxence Melo (Mmiliki wa Jamii Forum), Majjid Mjengwa (Mmiliki wa Blogu) na Josephat Isango (Mwandishi wa habari) walizungumza.

Siku ya pili, maadhimisho haya yalisheheni shughuli nyingi zikiwemo ujumbe mfupi wa salamu kutoka kwa wawakilishi wa mashirika ya UNESCO, MCT, UTPC, TMF, MOAT, TEF, TAMWA, KAS na TCRA.

Pia salamu mbalimbali zilitolewa na wageni maalumu ambao ni Balozi Filiberto CerianSe Bregondi (EU Head of Delegation), Alvero Rodriguez (UN System – Resident Coordinator)

Baada ya salamu hizo, mada mbalimbali ziliwasilishwa na Bw. Innocent Mungy kutoka TCRA, ambaye aliongelea kuhusu mitandao ya kijamii kwa ujumla na namna ilivyomkomboa mtanzania kupata taarifa kwa haraka zaidi

Mada nyingine iliwasilishwa na Bw. Ernest Sungura (Mkurugenzi wa TMF) ambaye mada yake ilihusu “Reflection on the media landscape in Tanzania”

Kadhalika mkutano uliunda kamati maalumu ambayo kwa pamoja walitoa maazimio ambayo yalipitishwa kwa sauti moja ili utekelezaji wake uanze mapema.

Maazimio hayo ni kama ifuatavyo:

Kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutosaini miswada miwili – Muswada wa Sheria ya Takwimu na Muswada wa Sheria za Makosa ya Mtandaoni.

Kumtaka Rais aagize serikali, kuchukua mara moja, hatua za kisheria kwa wanaotenda jinai dhidi ya vyombo vya habari na wanahabari – matukio ambayo yameonekana zaidi katika kipindi cha miaka 10 sasa.

Kuwashauri wamiliki wa vyombo vya habari wachukue jukumu la kutoa elimu zaidi na kukuza maarifa na stadi kwa waandishi wanaowaajiri.

Waandishi wa habari watambue umuhimu wa kujiendeleza kitaaluma ili wawe na weledi na umahiri unaowapa heshima ya kitaaluma mbele ya waajiri wao.

Kuwashauri wamiliki wa vyombo vya habari watekeleze haki za wafanyakazi wao, ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara kwa wakati; na kwa viwango vilivyokubaliwa;  na angalau kwa kiwango cha mishahara elekezi kutoka serikalini. Haki hizi ni pamoja na mikataba ya ajira, usalama kazini, matibabu na likizo.

Waandishi wa habari watumie mtandao wa intaneti kwa ajili ya kupata taarifa zaidi; lakini wafanye hivyo kwa uangalifu kwani siyo kila kitu mtandaoni ni cha kweli na sahihi.

Wamiliki wa vyombo vya habari na wahariri waweke mipango mahususi ya kutafuta na kuajiri wataalam wa matumizi ya mitandao ili kufunza waandishi wa habari, matumizi bora ya mitandao, ikiwa ni pamoja na usalama wa taarifa  wanazopokea, wanazoweka na wanazopitisha kwenye mitandao.

Wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanazingatia usawa wa jinsia katika ajira na mgawanyo wa majukumu; na wahariri waone kuwa ni wajibu wao kulea na kukuza vipaji vya waandishi wanawake na hasa wanaotoka vyuoni.

Kamati kushauri kila chombo cha habari kijenge maktaba na hifadhi nyingine za nyaraka – mtandaoni na katika chumba/jumba maalum – ili kurekodi historia ya watu na matukio, siku hadi siku kupitia vyombo vya habari, kwa matumizi ya marejeo ya sasa na baadaye. Aidha, vyombo vya habari vitumike kueneza utamaduni wa nchi badala ya kuwa vipaza sauti vya utamaduni wa nchi za nje.

mjumbe wa bodi ...
mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya utpc bw.deo nsokolo akichangia mada katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya utpc bw.deo nsokolo akichangia mada katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Waandishi wa habari maveterani waunde Jukwaa litakalowezesha kuwatambulisha waliko ili vyombo vya habari na waandishi binafsi, waweze kuwafikia kwa urahisi na kuwatumia kupata maarifa zaidi kwa maendeleo yao na taaluma.

Waandishi wa habari wafungue kesi ya madai mahakamani dhidi ya serikali, kuhusu kifo cha mwandishi Daudi Mwangosi aliyeuawa mikononi mwa polisi.

Wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri na wadau wa habari waliohudhuria maadhimisho ya leo ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, wanaahidi kusimama pamoja, kupigania utekelezaji wa maazimio haya.

Maazimio yote haya yatawasilishwa na kamati iliyoundwa ambayo mwenyekiti wake ni Bw. Ndimara Tegambwage.

makamu wa rais ...
makamu wa rais wa utpc bi. jane mihanji akisisitiza jambo kuhusu shughuli zinazofanywa na utpc katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani makamu wa rais wa utpc bi. jane mihanji akisisitiza jambo kuhusu shughuli zinazofanywa na utpc katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani

Wajumbe wengine wa kamati hii ni Bw. Abubakar Karsan, Bw. Simoni Berege , Bw. Richard Shaba, Bi. Valerie Msoka, Bw. Buibwa Said na  Bw. Mac Demelo.

News Archive

Our Videos

video