• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Klabu mpya ya mkoa wa simiyu yazinduliwa rasmi

uzinduzi

Pichani ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Ponsiano Nyami (katikati) akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ofisi na Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo. ( wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan (Kushoto) Ni mratibu wa Simiyu Press Club (SMPC) Frank Kasamwa.

Serikali ya mkoa wa Simiyu, imeahidi kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa habari ya Simiyu (SMPC), kuendeleza tasnia ya habari mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Elaston Mbwillo, katika sherehe za uzinduzi wa Klabu hiyo, zilizofanyika mjini Bariadi, mapema mwezi Julai.

“Nawaomba muwaandikie wadau wote hapa mkoani, ili waifahamu klabu yenu na shughuli mnazofanya”, alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika hotuba yake, iliyosomwa na Mheshimiwa Ponsiano Nyomi, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, aliwataka waandishi wa habari kuandika habari za kweli, zilizofanyiwa uchunguzi wa kina.

Awali Mratibu wa klabu hiyo, Frank Kasamwa, aliishukuru UTPC, kwa kuiwezesha  SMPC kusajiliwa, kupata vitendea kazi na kulipia ofisi.

Akisoma risala, Katibu wa SMPC, Samweli Mwanga alitaja changamoto zinazowakabili waandishi wa habari mkoani humo.

Changamoto hizo ni kutopewa ushirikiano na watendaji serikalini, kutukanwa na kubezwa na baadhi ya wadau.

Changamoto zingine ni ukosefu wa vitendea kazi kama kompyuta, kamera, meza na viti.

Katika sherehe fupi za uzinduzi wa klabu hiyo, wadau walichangia jumla ya Tsh 3,095,000/= ambazo ahadi zilikuwa ni Tsh 2,770,000/= na taslimu Tsh 325,000/=.

News Archive

Our Videos

video