• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Klabu ya waandishi wa habari simiyu yapata viongozi wapya

 Viongozi wapya wa Simiyu Press Club
 Viongozi wapya wa Simiyu Press Club

KLABU ya waandishi wa habari mkoa wa Simiyu (SMPC) imefanya mkutano wake wa kwanza wa uchaguzi na kupata viongozi wapya kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwanzoni mwa mwaka huu.

Mkutano huo wa uchaguzi uliofanyika tarehe 1/8/2015, ulisimamiwa na Bw. Victor Maleko afisa programu anayeshughulikia masuala ya klabu kutoka kutoka Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Pamoja na kwamba uchaguzi ulikuwa ndio ajenda muhimu ya mkutano huo, lakini pia marekebisho ya Katika ya SMPC ilikuwa ni moja ya ajenda ya mkutano huo.

Katiba ya klabu hiyo ilifanyiwa marekebisho katika maeneo mbalimbali ikiwemo sifa za mwanachama na viwango vya ada za kila mwaka kwa mwanachama.

Baada ya marekebisho hayo, ilifika ajenda ya uchaguzi ambapo uchaguzi huo ulifanyika kwa amani na utulivu na kwa kufuata misingi ya katiba na sheria za uchaguzi za klabu hiyo.

Wanachama halali walioshiriki uchaguzi huo kwa kupiga na kupigiwa kura walikuwa 11, na kura zilipigwa kwa namna mbili tofauri, moja ni kwa njia ya kura za NDIYO na HAPANA kwa nafasi zenye mgombea mmoja mmoja na njia nyingine ni kwa kuandika jina la mgombea kwa nafasi zenye wagombea zaidi ya mmoja.

Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifutavyo, Bw. Frank Kasamwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Bw. Paschal Michael alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, Bw. Samwel Mwanga alichaguliwa kuwa Katibu Mtendaji na Bi. Costantine Mathias Katibu Mtendaji Msaidizi.

Wengine ni pamoja na Bi Happy Severine aliyeshinda nafasi ya Mtunza Hazina, Bi Neema Rubein, Mtunza Hazina Msaidizi na Wajumbe watano wa kamati tendaji ni pamoja na BW. Derick Milton, Bw. Faustine Fabian, Bw. Alua Ujuku, Bw. Faraja Mohamed na Bi. Anitha
Balingilaki.

Uchaguzi huu umefanyika mara baada ya kamati ya muda iliyokuwa ikiendesha klabu hii kumaliza muda wake na hivyo kupisha uchaguzi kufanyika.

News Archive

Our Videos

video