• Font size:
  • Decrease
  • Reset
  • Increase

Events Calendar

June 2017
S M T W T F S
28 29 30 31 1 2 3
4 5 6 7 8 9 10
11 12 13 14 15 16 17
18 19 20 21 22 23 24
25 26 27 28 29 30 1

Mkutano wa nigf kufanyika mwezi septemba

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya maandalizi ya NIGF Bw
Mwenyekiti wa Kamati kuu ya usimimazi ya NIGF, Bw. Kenneth Simbaya

Kamati kuu ya usimamizi wa baraza linaloshughulikia masuala ya matumizi ya mtandao wa intaneti nchini (NIGF Steering Committee) imepanga rasmi tarehe ya mkutano wa kitaifa wa masuala ya intanenti (NIGF) ambao sasa utafanyika tarehe 11/9/2015 jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati kuu ya usimimazi ya NIGF, Bw. Kenneth Simbaya, alisema kuwa Kamati hiyo inayo wajibu mkubwa wa kuhakikisha mkutao huo unafanyika ili kutoa fursa kwa taasisi nyingine kupata uwelewa zaidi wa masuala haya intaneti hasa ikizingatiwa nchi yetu bado ipo nyuma sana kuhusu masuala mazima yanayohusiana na matumizi ya intaneti.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilichokaa tarehe 14/8/2015, kimefanya maamuzi mengine ikiwemo kuandaliwa kwa makubaliano maalumu ya utendaji kazi kati ya Kamati hiyo kuu na UTPC ambayo ni sekretarieti inayotekeleza maamuzi yote yanayofanywa na kamati hiyo.

Mbali na hilo, kamati hiyo pia imefanya uchambuzi makini wa mada mbalimbali ambazo zitatolewa na wadau katika mkutano huo wa kitaifa wa tarehe 11/9/2015.

Mada hizo, zilitolewa na Dr. Jim Yonaz ambaye ni mkufunzi wa chuo cha biashara cha IFM Dar es Salaam.

Alieleza kuwa, mada hizo zimechaguliwa kwa kuzingatia mambo muhimu na ya msingi ambayo wadau wengine wangependa kufahamu kuhusu matumizi ya mtandao wa intaneti na ambayo yatakuwa na manufaa kwa taifa zima.

“Uelewa kuhusu masuala ya matumizi ya mtandao wa intaneti ni vyema ukatolewa mapema kwa mwananchi wa kawaida hasa ikizingatiwa kasi ya ukuaji wa teknolojia ni kubwa ikilinganishwa na uelewa wa watumiaji wenyewe, hivyo mada hizi ni muhimu zikaelezwa kwa kina na wahusika” Aliongeza Dr. Yonaz

Mkutano huo wa kitaifa utapanga mambo mengine ikiwemo mada zitakazotolewa kwenye mkutano wa nchi za Afrika Mashariki (EAIGF) ambao umepangwa kufanyika tarehe 24 na 25 mwezi Septemba mjini Kampala Uganda na Dunia (UNIGF), ikiwemo orodha wadau watakotakiwa kuhudhuria mikutano hiyo ya kimataifa.

News Archive

Our Videos

video