Home About Press Clubs Multimedia Contact Us Staff Mail

Maazimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yafanyika Mwanza kwa kuwashirikisha wanahabari

11-Dec-19

Katika muendelezo wa maadhimisho siku ya Haki za Binadamu Duniani ambayo hufanyika kila tarehe 10 Disemba, Unesco, Umoja wa Mataifa na UTPC leo wamekutana na waandishi wa habari mkoani Mwanza kupitia Mwanza Press Club lengo likiwa ni kujadiliana kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kutetea na kulinda haki za wanawake na watoto lakini pia kushughulikia suala zima la unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Pamoja na mambo mengine, katika kikao hicho wamekubaliana mambo kadha wa kadha moja ikiwa ni UNESCO kwa kushirikiana na UTPC kuandaa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kwenye eneo la Haki za Binadamu, kuitumia mikutano ya wadau inayofanyika kwenye klabu za waandishi wa habari na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ili kuzungumza kuhusu namna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inavyofanya kazi, lakini pia kuandaa kuongeza nguvu kwenye eneo la mafunzo ya usalama kwa mwandishi wa Habari.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika ofisi za UTPC, kitabu/muongozo maalumu wa kuandika habari za unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike kilizinduliwa rasmi.