Home About Press Clubs Multimedia Contact Us Staff Mail

MPC KUFAIDIKA NA VIFAA KINGA DHIDI CORONA TOKA EWURA

02-Jun-20

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa MPC leo Mei 13, 2020 imepokea vifaa kinga toka Mamlaka ya kudhibiti nishati na maji ya Kanda ya Ziwa EWURA.

Akikabidhi vifaa hivyo, Meneja wa EWURA kanda ya Ziwa Bw. George Mhina amesema kuwa Mamlaka hiyo imechukua hatua ya kuwaunga mkono Waandishi wa Habari kutokana na jitihada zao thabiti za kuhakikisha wanaendelea kuhabarisha umma dhidi ya mapambano ya ugonjwa huu wa Corona.

Hata hivyo, ameihakikishia Klabu ya Waandishi wa Habari kuendelea kuiunga mkono na kuwa walichokikabidhi leo sio mwisho, bali wakati wowote MPC itakapohitaji msaada isisite kubisha hodi, nao kama Mamlaka itatoa ushirikiano.

Vifaa Kinga vilivyokabidhiwa kwa MPC ni Barakoa 100, Ndoo kubwa 7 za Lita 20, vitakasa mikono chupa ndogo 36, boksi 1 la tissue lenye pakiti 20 na Sabuni 12 za kunawia mikono.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza Bw. Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa msaada walioupatia klabu na kueleza kuwa vifaa kinga hivyo vitagaiwa kwa waandishi wote wa Habari bila kubagua mwanachama na asiye mwanachama wa MPC.