UTPC YAPEWA TUZO

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia,wazee na watoto Mh. Dr.Doroth Gwajima amekabidhi tuzo Kwa Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC Deogratius Nsokolo Kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari nchini na UTPC katika kuhamasisha na kuandika habari kuhusu Mfuko wa Taifa wa bima ya afya tangu ulipoanzishwa mwaka 2001, ni katika maadhimisho ya miaka 20 ya NHIF yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bernard Konga amesema tuzo hiyo ni ishara ya kutambua mchango wa waandishi katika kuelimisha umma kuhusu Mfuko wa Taifa wa bima ya afya na kwamba wataendelea kutumia taasisi za kihabari na waandishi katika maboresho ya mfuko.