Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC), imepokea vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Hatua hiyo imekuja baada ya The Desk and Chair Foundation kuwa na mazungumzo na klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza juu namna gani taasisi hizo zinaweza kusaidiana kuwalinda waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza.
Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa Mwenyekiti wa taasisi ya the desk and chair foundation-Sibtain Meghjee, amesema kuwa taasisi yake inatambua umuhimu wa waandishi wa habari na hivyo imeamua kusaidia vifaa vya kujikinga ili waandishi waweze kufanya kazi kwenye mazingira salama.
Meghjee amesema kuwa, waandishi wana wajibu mkubwa wa kuielimisha jamii kwenye wakati huu wa janga la corona.
Nae Mwenyekiti wa Mwanza wa waandishi wa klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC)Bwana Edwin Soko alisema kuwa, kitendo kilichoonyeshwa na the Desk and Chair Foundation ni kitendo cha kizalendo, kwa kinalenga kuwalinda waandishi wa habari, ambao wanafanya kazi kwenye mazingira ya hatari wakati huu wa janga la ugonjwa wa corona.
Mwenyekiti Soko amewaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kusaidia waandishi wa habari kwa wakatì huu wa janga la corona kwa kuwa, uhitaji wa vifaa vya kujikinga ni mkubwa.
Pia alisema MPC inawajibu wa kuhakikisha waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza wanakuwa salama wakati wote na MPC imebeba dhamana kubwa ya kuwalinda usiku na mchana na vifaa hivyo vitawanufaisha waandishi wote wa Mkoa wa Mwanza .
Vifaa vikivyotolewa ni pamoja na gloves, barakoa,vitiririsha maji, sabuni za maji na vitakasa mikono.