MAHAKAMA KUU YA RUFAA MWANZA ITATOA MAAMUZI YA RUFAA YA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI (MSA) 2016 SIKU CHACHE ZIJAZO

Leo Februari 19, 2021  Mahakama ya Rufaa Mkoani Mwanza, imesikilizwa  kesi ya rufaa ambayo ilifunguliwa na UTPC na Halihalisi publishers dhidi ya sheria ya huduma za vyombo vya Habari (MSA), 2016 baada ya Mahakama kuu kutoa hukumu yake mwaka 2018.

 

Katika rufaa hii, UTPC na Halihalisi wamewakilishwa na mawakili Edwin Aron Hans na Jeremiah Mtobesya.

Mawakili wa UTPC na Halihalisi waliwasilisha rufaa hiyo mbele ya majaji wa Mahakama ya rufaa mkoani Mwanza na mbele ya mawakili wa serikali.

 

Mwaka 2017, UTPC na Halihalisi Publishers walifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mwanashiria Mkuu wa Serikali kupinga sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ambayo inakiuka misingi ya kikatiba kuhusu Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Vyombo vya Habari.

 

Baada ya majadiliano marefu, Majaji wa rufani wameeleza kutoa maamuzi ya rufaa hiyo baada ya siku chache kutoka leo.