Afisa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo ya Sweden Nchini (Sida) Bw. Stephen Chimalo, ametembelea Klabu za Waandishi wa Habari za mikoa ya SHINYANGA, KAGERA, GEITA, TABORA na KIGOMA, ili kujionea maendeleo ya klabu hizo ambazo zinajengewa uwezo kupitia mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) chini ya usimamizi Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
katika zaira hiyo, Bw. Stephen amejionea ushirikiano mzuri unaoonyeshwa na waandishi wenyewe kwa wenyewe katika kupigania uhuru wa habari lakini pia nafasi ya vyombo vya habari huru katika kuuhabarisha umma. Pia amesikia jinsi waandishi hao wanavyonufaika na msaada unaotolewa na Sida kupitia UTPC hasa kwenye eneo la Mafunzo, Ziara za Mafunzo na Vifaa.
Mbali na hilo amejionea namna Kagera Press Club walivyoweka nia ya kuongeza wigo kufahamika katika mipaka ya Rwanda, Burundi na Uganda.
Alimaliza ziara yake kwa kutembelea Kigoma Press Club ambapo amefurahishwa kuona hadhi ya ofisi ya Kigoma Press Club ambayo inalingana na kodi inayolipwa chini ya ufadhili wa Sida lakini pia ushirikiano uliopo kati ya Viongozi na wanachama wake.
#PressClubsKwaMaendeleoYaMkoa