Mlezi wa MPC Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella

Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mwanza
(MPC), ni Klabu iliyosajiliwa chini ya Sheria ya "Society Act" tarehe
9 Disemba 1994 kwa usajili wa namba S.109 na kufanya kazi ndani
ya Mkoa wa Mwanza ikiwa lengo kuu ni kuchochea maendeleo ya
Mkoa wa Mwanza.

Ndugu wanachama, Kamati Tendaji ya Klabu inapenda kuwataarifu
kuwa, kwa sasa Klabu yetu imempata mlezi wa ambaye atahusika
na suala zima la kuilea na kuishauri kwa muda wote kama neno
tafsiri ya mlezi lilivyo

Mlezi huyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John
Mongella

Hatua hiyo imeambatana na ziara iliyofanywa na viongozi wa klabu
kwa Mkuu wa Mkoa Oktoba 11, 2019.

Mwisho tunamshukuru Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mheshimiwa John
Mongella kwa kukubali kuwa mlezi wa klabu yetu.

Imetolewa na Kamati Tendaji MPC tarehe 11:10:2019