Kwa kuona umuhimu wa matibu kwa wanachama wa klabu za waandishi wa habari, UTPC ilifanya mazungumzo na mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) kwa lengo la kutengeneza kifurushi au mpango maalumu wa matibabu kwa waandishi wa habari ambao ni wanachama wa klabu za waandishi wa habari.
Katika mazungumzo hayo, UTPC na NHIF walikubaliana kwamba kila mwanachama atachangia Tsh. 100,000/= kwa mwaka akiwa peke yake bila mtegemezi, na kama atahitaji kuweka mtegemezi ambaye umri wake ni zaidi ya miaka 18 atachangiwa Tsh. 100,000/= na mtoto atachangiwa Tsh. 50,400/= kwa mwaka.
Baada ya mazungumzo hayo kukamilika, klabu zote zilijulishwa kuhusu fursa hiyo ya matibabu ambayo ilitengenezwa mahususi kwa ajili ya waandishi wa habari.
Klabu zilianza kuhamasisha wanachama wake na kukusanya michango kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya.
Jumla ya klabu 11 zimekamilisha chakato wa kuwakatia bima ya afya wanachama wake kama inavyoonekana katika orodha hapa chini
Central Press Club
Geita Press Club
Kigoma Press Club
Mwanza Press Club
Mbeya Press Club
Rukwa Press Club
Shinyanga Press Club
Simiyu Press Club
Zanzibar Press Club
Katavi Press Club
Dar City Press Club
Kwa sasa hakuna klabu itakayoendelea na mchakato huu mpaka mwakani. Hivyo klabu ambazo hazijakamilisha mchakato huu, zitapewa nafasi ya kukamilisha shughuli hii mwaka 2021.