- Nov 29,2019
- General
Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC yapitisha Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2020
Bodi ya wakurugenzi ya UTPC, ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Rais wa UTPC Bwana Deo Nsokolo, imefanya vikao vyake vya mwisho wa mwaka na moja ya ajenda kubwa ilikuwa ni kupitisha Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2020.
Katika kikao hicho ambacho kilitanguliwa na vikao vya Kamati za Fedha na Mipango pamoja na Maadili na Mafunzo, pia kilipitisha ajira ya Ofisa Ugavi wa UTPC ambaye atakayeshughulikia masuala yote manunuzi.
Pamoja na mambo mengine Bodi ya Wakurugenzi imejadili na kupitisha masuala mengine kadhaa ikiwemo, mchakato wa kuandaa Mpango Mkakati 2021 – 2025, Mkakati wa kujenga uwezo wa Klabu kwenye usimamizi na udhibiti wa fedha, Orodha ya Makampuni ya utoaji huduma ambayo yatafanya kazi na UTPC kwa mwaka 2020.
Bodi hii pia imejadili suala la athari za nakisi kwenye bajeti zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi zake kwa miaka minne iliyopita, lakini pia Bodi imepitisha taarifa ya maendeleo ya mafunzo mpaka kufikia mwezi Novemba mwaka huu.
Kikao kimemalizika tarehe 20 Novemba 2020