Event

Latest from our posts

Discover the newest articles and updates from our blog, covering a variety of engaging topics.

Blog

UTPC YATOA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UGONJWA WA COVID19 KWA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.

Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC), umeanza kutoa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 kwa klabu za waandishi wa habari na wanachama wake nchini kote.

 

Maamuzi haya yamefikiwa ili kuendelea kutoa ulinzi kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari wa mbele kutafuta na kutoa habari kwa wadau wote nchini hasa katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugongwa wa COVID19.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Barakoa, vitakasa mikono, ndoo za kuwekea maji, karatasi laini (Tishu), glavu (gloves) na vingingenevyo. Vifaa hivi vimetolewa kwa mwandishi mmoja mmoja na vingine vimetolewa kwa ajili ya ofisi za klabu.

 

Pamoja na mambo mengine, UTPC inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali ambao wameendelea kuzisaidia klabu za waandishi habari kwa kutoa vifaa mbalimbali vya kujilinda na maambukizi haya ugonjwa wa COVID19. UTPC inathamini sana mchango wa wadau wote walioshiriki kikamilifu kuhakikisha mwandishi wa habari anakuwa salama ili aendelee kuuhabarisha umma katika kipindi hiki kigumu ambapo jamii inahitaji taarifa sahihi ili kuongeza uelewa na usalama wao.

 

Hata hivyo UTPC inapenda kuwasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuchukua tahadhari za kujilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 kwa kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo Wizara ya Afya na WHO.

Read More
Blog

Maazimisho ya Siku ya Haki za Binadamu yafanyika Mwanza kwa kuwashirikisha wanahabari

Katika muendelezo wa maadhimisho siku ya Haki za Binadamu Duniani ambayo hufanyika kila tarehe 10 Disemba, Unesco, Umoja wa Mataifa na UTPC leo wamekutana na waandishi wa habari mkoani Mwanza kupitia Mwanza Press Club lengo likiwa ni kujadiliana kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kutetea na kulinda haki za wanawake na watoto lakini pia kushughulikia suala zima la unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto.

Pamoja na mambo mengine, katika kikao hicho wamekubaliana mambo kadha wa kadha moja ikiwa ni UNESCO kwa kushirikiana na UTPC kuandaa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kwenye eneo la Haki za Binadamu, kuitumia mikutano ya wadau inayofanyika kwenye klabu za waandishi wa habari na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, ili kuzungumza kuhusu namna Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inavyofanya kazi, lakini pia kuandaa kuongeza nguvu kwenye eneo la mafunzo ya usalama kwa mwandishi wa Habari.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika katika ofisi za UTPC, kitabu/muongozo maalumu wa kuandika habari za unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wa kike kilizinduliwa rasmi.

Read More
Blog

Afisa Miradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) atembelea Klabu za Waandishi wa Habari

Afisa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo ya Sweden Nchini (Sida) Bw. Stephen Chimalo, ametembelea Klabu za Waandishi wa Habari za mikoa ya SHINYANGA, KAGERA, GEITA, TABORA na KIGOMA, ili kujionea maendeleo ya klabu hizo ambazo zinajengewa uwezo kupitia mradi unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (Sida) chini ya usimamizi Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

katika zaira hiyo, Bw. Stephen amejionea ushirikiano mzuri unaoonyeshwa na waandishi wenyewe kwa wenyewe katika kupigania uhuru wa habari lakini pia nafasi ya vyombo vya habari huru katika kuuhabarisha umma. Pia amesikia jinsi waandishi hao wanavyonufaika na msaada unaotolewa na Sida kupitia UTPC hasa kwenye eneo la Mafunzo, Ziara za Mafunzo na Vifaa.

Mbali na hilo amejionea namna Kagera Press Club walivyoweka nia ya kuongeza wigo kufahamika katika mipaka ya Rwanda, Burundi na Uganda.

Alimaliza ziara yake kwa kutembelea Kigoma Press Club ambapo amefurahishwa kuona hadhi ya ofisi ya Kigoma Press Club ambayo inalingana na kodi inayolipwa chini ya ufadhili wa Sida lakini pia ushirikiano uliopo kati ya Viongozi na wanachama wake.

 #PressClubsKwaMaendeleoYaMkoa

Read More
Blog

Wito watolewa kwa Waandishi wa Habari kujiendeleza kielimu.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba amewataka waandishi wa habari kote nchini kujiendeleza kielimu ili kukidhi matakwa ya kisheria, kwani TCRA itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa waandishi wote watakaokosa vigezo, lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha tasnia ya habari nchini, lakini pia kusimamia maudhui na kuleta mshikamano na amani nchini.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika Mkutano wa majadiliano kati ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mwanza yaliyoandaliwa na Klabu Ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC).

Aliongeza kuwa TCRA itaendelea kuchukua hatua kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa maudhui mitandaoni, ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi vya kisasa na raslimali watu wa kutosha ili kuleta ufanisi kwenye sekta ya mawalisiano.

Pamoja na hayo, Bw. Kilaba alisema kuwa sheria ya habari ya mwaka 2016 inamtaka kila mwandishi kuwa na elimu ya kuanzia ngazi ya “Diploma” ambapo serikali imetoa kipindi cha mpito cha muda wa miaka 5 kitakachondelea hadi tarehe 31 Disemba, 2021, ili kutoa nafasi kwa kila mwandishi kujiendeleza kielimu na kufika ngazi ya Diploma.

Hata hivyo Bw. Kilaba aliwaambia waandishi hao kuwa, TCRA ilitoa kumbusho kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuzingatia matakwa ya sheria na masharti ya leseni za utangazaji kwa kuhakikisha kuwa wanaotangaza katika vyombo vyao wanakuwa na vigezo vya kitaaluma kama waandishi wa habari.

Naye Mkurugenzi wa UTPC Bw. Abubakar Karsan, alitoa wito kwa waandishi wa habari kuhakikisha wanafuata sheria wakati wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.

Pamoja na wito huo, Bw. Karsan alitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa TCRA kwa kukubali kushiriki kwenye mkutano huo maalumu kwa waandishi wa habari mkoa wa Mwanza.

Pia aliongeza kuwa, mwaka 2020 UTPC imeandaa mpango maalumu wa kuziwezesha klabu zote 28 nchini kusajili blog zao ili iwe rahisi kuchapisha habari nyingi za mkoa husika na kusaidia kuleta maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla. 

Read More
Blog

Sida na UTPC wakutana kujadili Mpango Kazi na Bajeti wa mwaka 2020.

Katika kikao kilichofanyika jana katika ofisi za UTPC Mwanza, Ofisa wa Sida Bw. Stephen Chimalo, alikutana na Sekretarieti ya UTPC ikiongozwa na Mkurugenzi wake Bw. Abubakar Karsan ili kujadili Mpango Kazi na Bajeti ambao unafadhiliwa na Sida kupitia Mpango Mkakati 2016 – 2020.

Mpango kazi huu wa 2020, ulijadiliwa kwa kulinganishwa na Mpango Kazi 2019 ambao unamalizika mwezi Disemba mwaka huu.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kilijadili kuhusu Mpango Kazi wenye shughuli za ziada ambazo zitaombewa fedha kwa mfadhili mwengine.

Read More
Blog

Rais wa UTPC afungua mafunzo kwa waandishi wa habari Dodoma

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Bwana Deo Nsokolo, amefungua rasmi mafunzo ya uandishi wa habari za Vijijini kwa wanachama wa Klabu za Waandishi wa habari nchini yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Akifungua mafunzo hayo, Bwana Deo Nsokolo  amesema kwamba mafunzo wanayokwenda kupewa waandishi hawa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za UTPC katika Mpango Mkakati wake 2016 - 2020, ambao unaelekea mwishoni.

Alisema kwamba UTPC inapenda kuona mafunzo haya yanafanyiwa kazi kwa waandishi wa habari kuandika habari ambazo zitachangia maendeleo ya mikoa husika  lakini pia kupata waandishi wa habari wabobezi kwenye eneo wanalopata mafunzo.

Aliongeza kwamba UTPC inapenda kuona katika mafunzo haya kila mtu anapata nafasi ya kushiriki lakini pia kuwepo na mchanganyiko wa wanachama na viongozi wa klabu na ndio maana mafunzo haya yanatolewa kwa utaratibu wa wanachama kuomba na kuchaguliwa.

Akijibu swali la Bwana Adam Malima, kuhusu nafasi ya UTPC katika kutetea ajira za waandishi wa habari na mikataba yao, Rais wa UTPC alisema kwamba suala la ajira ni tatizo kwenye tasnia ya habari, ila zipo jitihada ambazo zinafanywa na UTPC kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kihabari ili kwa pamoja kutatua tatizo hili.

“Jambo la kufanya ni kwamba wamiliki wa vyombo vya habari wawathamini waandishi wao kwa kuwapa mikataba na kuwalipa vizuri ili kuboresha tasnia ya habari lakini pia kwa kufanya hivyo maadili ya uandishi wa habari yatazingatiwa kwa kuwa kila mwandishi atakuwa na uhakika wa ujira wake” -  Alisema Deo Nsokolo

Akizungumzia suala la maadili kwa wandishi wahabari, Bwana Deo Nsokolo aliwataka waandishi wa habari kutotumia tasnia ya habari kwa kutekeleza uovu wao.

“Msitumie tasnia ya habari kufanya uovu au kujificha nyuma ya uandishi wa habari kwa uovu wenu mkitegemea UTPC itawatetea, UTPC haitetei uandishi wa habari usiongizatia maadili na taaluma Kila mwandishi afanye kazi yake kwa kufuata maadili ya uandishi wa habari.” – Deo Nsokolo 

Pamoja na mambo mengine, Rais alisema kwamba, vyombo vya habari vimejaa hofu kubwa na waandishi wamekosa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa uthubutu.

Bwana Nsokolo alizungumia huduma zinazotolewa na UTPC kwa Klabu za Waandishi wa habari,  alisema kwamba UTPC inafanya mambo mengi ukiachilia mbali mafunzo kwa waandishi wa habari. Alizitaja huduma hizo kamna vile kodi ya pango kwa Press Clubs zote, Internet, Maji na Umeme, vifaa kama vile compyuta na Kamera ambavyo vinapelekwa moja kwa moja kwenye klabu.

“Kwenye klabu zenu mnapashwa kuwa na intaneti wakati wote, lakini pia Klabu za waandishi wa habari zinapashwa kuwa ni ofisi zenye hadhi kwa kuwa UTPC inalipa kodi za ofisi hizo”

Rais alimaliza kwa kusema kwamba, mwaka 2020 ni ukomo wa ungozi kwa viongozi wa klabu hivyo UTPC na klabu zake wanategemea kufanya uchaguzi wa viongozi wake kwa mwaka huo. Aliwatia moyo washiriki hao kwamba wasisite kushika nafasi ya uongozi kwenye klabu au katika Bodi ya Wagurugenzi ya UTPC.

“Ikifika wakati wa uchaguzi hakikisheni mnachagua viongozi wazuri wa klabu zenu ili klabu zenu ziendelee kusimama” – Alisema Deo

Mafunzo mengine yaliyofanyika mkoani Dodoma katika wiki hiyo ni Mafunzo ya uandishi wa habari za Mazingira na mafunzo ya uandishi wa habari za Jinsia.

Read More