Event

Latest from our posts

Discover the newest articles and updates from our blog, covering a variety of engaging topics.

Blog

KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI 17 ZAKAMILISHA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAO

Mkutano Mkuu wa UTPC uliofanyika tarehe 15 na 16 Septemba 2017 mkoani Tanga, ulifanya mabadiliko ya katiba yake kuhusu muda wa ukomo wa viongozi wa klabu kuwapo madarakani kutoka miaka mitatu hadi miaka mitano kama inavyoonekana katika katiba ya UTPC kipengele namba 15 (C).

 

Kwa mujibu wa azimio namba 8.3 la Mkutano Mkuu wa dharura uliofanyika Dodoma terehe 23/08/2013, wajumbe waliazimia kwamba klabu zote zifanye uchaguzi wao mapema kabla ya uchaguzi wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambapo wajumbe wake huchaguliwa kutoka miongoni mwa viongozi wa juu wa  Klabu za Waandishi wa Habari.

 

Katika kikao cha 33 cha Bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika tarehe 20/11/2019 mkoani Dodoma, kilipitisha azimio namba 5.2.4.1 ambalo lilizitaka klabu zote ziwe zimefanya uchaguzi wa viongozi wake mpaka kufikia tarehe 30 Juni 2020 ili kupisha uchaguzi wa Mkuu wa Serikali na uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC.

 

Hata hivyo kutoka na mlipuko wa ugonjwa wa COVID19, Bodi ilisogeza mbele muda wa chaguzi za klabu mpaka kufikia tarehe 30 Septemba 2020.

 

Baada ya maagizo haya kutolewa na Bodi ya Wakurugenzi, klabu zilianza kufanya chaguzi zake katika vipindi tofauti tofauti, na ifuatayo ni orodha ya klabu ambazo zimeshafanya chaguzi zake;

 

Central Press Club

Kigoma Press Club

Njombe Press Club

Mwanza Press Club

Geita Press Club

Songwe Press Club

Rukwa Press Club

Katavi Press Club

Mara Regional Press Club

Simiyu Press Club

Shinyanga Press Club

Mtwara Press Club

Lindi Press Club

Kagera Press Club

Mbeya Press Club

Arusha Press Club

Manyara Press Club  

 

Klabu zilizobaki bado zinaendelea na mchakato wa kufanya chaguzi zake na pindi wakatakapo maliza taarifa yake itaandaliwa.

Read More
Blog

KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI ZAANZISHA BLOGU

Bodi ya Wakurugenzi katika kikao chake namba 33 kilichofanyika Mkoani Dodoma tarehe 20/11/2019, kilifanya mabadiliko ya baadhi ya kasma za bajeti ya mafunzo ili fedha hizo ziende kusaidia uanzishwaji wa blogu za klabu za Waandishi wa Habari zilizopo mikoani.

 

Madhumuni ya kuanzishwa kwa blog hizi, ni kusaidia maendeleo katika mkoa husika kwa kuchapisha na kusambaza habari mbalimbali zinazoonyesha fursa zinazopatikana katika mikoa hiyo kupitia blog za klabu. Lakini pia blog hizi zitasaidia habari za vijijini kupata nafasi ya kusikika na kusomwa nchini kote.  

 

Mpaka sasa jumla ya klabu za waandishi wa habari 13 zimefanikiwa kusajili na kufungua blogu zao na zinafanya kazi. Klabu hizo ni kama ifuatavyo

 

Shinyanga Press Club – www.shinyangapress.blogspot.com

Geita Press Club – www.geitapress.blogspot.com

Kigoma Press Club – www.kigomapress.blogspot.com   

Central Press Club – www.centralpressclub.co.tz

Arusha Press Club – www.arushapressclub.blogspot.com  

Njombe Press Club – www.njombepress.blogspot.com

Katavi Press Club – www.katavipress.blogspot.com

Manyara Press Club – www.manyarapress.blogspot.com

Tabora Press Club – www.taborapress.blogspot.com

Iringa Press Club – IPC Mkombozi TV (YouTube channel) https://www.youtube.com/channel/UCposvKsTmu7E9_NC6WbLaCg/featured?disable_polymer=1

Rukwa Press Club – www.rukwapress.blogspot.com

Pemba Press Club – www.pembapress.club/portal/

Mwanza Press Club – www.mwanzapressclub.co.tz  

 

Klabu zilizobaki bado zinaendelea na usajili wa klabu zake na zitakapokuwa tayari taarifa yake itatolewa.

Read More
Blog

TANZIA  -  TAARIFA ZA KIFO CHA ALIYEKUWA MFANYAKAZI WA UTPC NDUGU JACOB KAMBILI

UTPC imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa mfanyakazi wa UTPC, ndugu Jacob Njayeje Kambili, kilichotokea katika hospitali ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Jacob Ngayeje Kambili alizaliwa tarehe 22 Oktoba 1953 na kufariki dunia tarehe 29 Julai 2020 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu alisumbuliwa sana ugonjwa wa Tezi Dume ambao ulimfanya kushindwa kuendelea kufanya kazi na UTPC na kuamua kustaafu rasmi mwaka 2018.

 

Marehemu Jacob Njayeje Kambili alikuwa ni mwandishi wa habari mkongwe aliyefanya kazi kwa umahiri na kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yake. Marehemu alifanya kazi na UTPC kwa kipindi kisichopungua miaka 7 na kabla ya hapo alifanya kazi na klabu ya waandishi wa habari Mwanza (Mwanza Press Club) akiwa kama Katibu wa klabu hiyo huku akiendelea na taaluma yake ya uandishi wa habari ambapo alifanya kazi kwenye vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini ikiwemo Gazeti la Daily News.

Marehemu Jacob Ngayeje Kambili alikuwa mcha Mungu mwenye upendo wa dhati kwa wafanyakazi wenzake lakini pia mkweli na mcheshi wakati wote.

Kwa niaba ya wanahabari wote Tanzania, UTPC inapenda kutoa pole kwa msiba huu mzito ambao umewagusa watu wengi ambao walifanya kazi na marehemu kwenye tasnia ya habari.

Mungu ailaze roho ya marehemu malaha pema peponi amina.

Read More
Blog

UTPC YATOA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UGONJWA WA COVID19 KWA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA.

Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC), umeanza kutoa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 kwa klabu za waandishi wa habari na wanachama wake nchini kote.

Maamuzi haya yamefikiwa ili kuendelea kutoa ulinzi kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa mstari wa mbele kutafuta na kutoa habari kwa wadau wote nchini hasa katika kipindi hiki cha maambukizi ya ugongwa wa COVID19.

 

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Barakoa, vitakasa mikono, ndoo za kuwekea maji, karatasi laini (Tishu), glavu (gloves) na vingingenevyo. Vifaa hivi vimetolewa kwa mwandishi mmoja mmoja na vingine vimetolewa kwa ajili ya ofisi za klabu.

 

Pamoja na mambo mengine, UTPC inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wadau mbalimbali ambao wameendelea kuzisaidia klabu za waandishi habari kwa kutoa vifaa mbalimbali vya kujilinda na maambukizi haya ugonjwa wa COVID19. UTPC inathamini sana mchango wa wadau wote walioshiriki kikamilifu kuhakikisha mwandishi wa habari anakuwa salama ili aendelee kuuhabarisha umma katika kipindi hiki kigumu ambapo jamii inahitaji taarifa sahihi ili kuongeza uelewa na usalama wao.

 

Hata hivyo UTPC inapenda kuwasisitiza waandishi wa habari kuendelea kuchukua tahadhari za kujilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 kwa kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wa afya ikiwemo Wizara ya Afya na WHO.

 

Read More
Blog

MPC KUFAIDIKA NA VIFAA KINGA DHIDI CORONA TOKA EWURA

Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa MPC leo Mei 13, 2020 imepokea vifaa kinga toka Mamlaka ya kudhibiti nishati na maji ya Kanda ya Ziwa EWURA.

Akikabidhi vifaa hivyo, Meneja wa EWURA kanda ya Ziwa Bw. George Mhina amesema kuwa Mamlaka hiyo imechukua hatua ya kuwaunga mkono Waandishi wa Habari kutokana na jitihada zao thabiti za kuhakikisha wanaendelea kuhabarisha umma dhidi ya mapambano ya ugonjwa huu wa Corona.

Hata hivyo, ameihakikishia Klabu ya Waandishi wa Habari kuendelea kuiunga mkono na kuwa walichokikabidhi leo sio mwisho, bali wakati wowote MPC itakapohitaji msaada isisite kubisha hodi, nao kama Mamlaka itatoa ushirikiano.

Vifaa Kinga vilivyokabidhiwa kwa MPC ni Barakoa 100, Ndoo kubwa 7 za Lita 20, vitakasa mikono chupa ndogo 36, boksi 1 la tissue lenye pakiti 20 na Sabuni 12 za kunawia mikono.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza Bw. Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa msaada walioupatia klabu na kueleza kuwa vifaa kinga hivyo vitagaiwa kwa waandishi wote wa Habari bila kubagua mwanachama na asiye mwanachama wa MPC.

Read More
Blog

MPC YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA(PPE) TOKA  TAASISI YA  THE DESK AND CHAIRS FOUNDATION

Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC), imepokea vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Hatua hiyo imekuja baada ya The Desk and Chair Foundation kuwa na mazungumzo na klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza juu namna gani taasisi hizo zinaweza kusaidiana kuwalinda waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza.

Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa Mwenyekiti wa taasisi ya the desk and chair foundation-Sibtain Meghjee, amesema kuwa taasisi yake inatambua umuhimu wa waandishi wa habari na hivyo imeamua kusaidia vifaa vya kujikinga ili waandishi waweze kufanya kazi kwenye mazingira salama.

Meghjee amesema kuwa, waandishi wana wajibu mkubwa wa kuielimisha jamii kwenye wakati huu wa janga la corona.

Nae Mwenyekiti wa Mwanza wa waandishi wa klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC)Bwana Edwin Soko alisema kuwa, kitendo kilichoonyeshwa na the Desk and Chair Foundation ni kitendo cha kizalendo, kwa kinalenga kuwalinda waandishi wa habari, ambao wanafanya kazi kwenye mazingira ya hatari wakati huu wa janga la ugonjwa wa corona.

Mwenyekiti Soko amewaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kusaidia waandishi wa habari kwa wakatì huu wa janga la corona kwa kuwa, uhitaji wa vifaa vya kujikinga ni mkubwa.

Pia alisema MPC inawajibu wa kuhakikisha waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza wanakuwa salama wakati wote na MPC imebeba dhamana kubwa ya kuwalinda usiku na mchana na vifaa hivyo vitawanufaisha waandishi wote wa Mkoa wa Mwanza .

Vifaa vikivyotolewa ni pamoja na gloves, barakoa,vitiririsha maji, sabuni za maji na vitakasa mikono.

Read More