Event

Latest from our posts

Discover the newest articles and updates from our blog, covering a variety of engaging topics.

Blog

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA

Mafunzo ya siku mbili kuhusu Ulinzi na Usalama kwa Mwandishi wa Habari, yamemalizika leo mkoani Dodoma ikiwa ni awamu ya pili kufanyika kwa mafunzo haya.
Washiriki 20 kutoka klabu za waandishi wa habari nchini wameshiriki mafunzo haya ambayo yameongozwa na Mwandishi mbobezi Bw. Neville Meena kutoka Jukwaa la Wahariri.
Akifunga mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya UTPC Bw. Mussa Yusuph amewataka waandishi waliopata mafunzo haya kuzingatia kile walichofundishwa kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kufahamu mipaka ya kazi yao ili kulinda maisha yao kwakuwa waandishi wanapopata matatizo na kushindwa kufanya kazi, inayoathirika zaidi ni jamii ambayo inamtegemea Mwandishi wa Habari kupata taarifa sahihi ili mwisho wa siku jamii hiyo ifanye maamuzi sahihi.
Pamoja na mambo mengine Bw. Mussa aliwashukuru wafadhili wa mradi huu ambao ni shirika la IMS kutoka nchini Denmark ambao wameiamini taasisi ya UTPC na kuamua kufanya nayo kazi.
Mpaka kufikia mwisho wa mradi huu, waandishi wa Habari 100 wanatakiwa wawe wameshapata mafunzo haya ya Ulinzi na Usalama.
Read More
Blog

SERIKALI YAANZA KUJENGA MAHUSIANO ENDELEVU NA WAANDISHI WA HABARI

Mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo na msemaji mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa amesema Serikali imeanza kujenga mahusiano endelevu na waandishi wa habari na taasisi zinazomia waandishi wa habari nchini, hatua ambayo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi.
Msigwa ameyasema hayo alipokutana na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari nchini UTPC Deogratius Nsokolo mjini Singida.
Msigwa amesema Serikali inatambua mchango wa waandishi wa habari na Press Club nchini katika kusimamia maadili na kusaidia maendeleo katika mikoa mbalimbali na ndio maana ameamua kuweka utaratibu wa kutoa taarifa za Serikali Kwa kukutana na waandishi katika mikoa mbalimbali.
Amesema hatua hiyo inawapa fursa waandishi kuuliza juu ya mkoa wao na Taifa.
"Nimemualika Rais wa UTPC hapa Singida ili kuonyesha azma ya serikali kuwathamini na kuwatumia wandishi wa habari katika mikoa yote kueleza masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali lakini Serikali kupata mrejesho kupitia kwao Kwa kuwa ndio wapo karibu zaidi na wananchi" alisema Msigwa.
Kwa upande wake Rais wa muungano wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo alimshukuru Msemaji mkuu wa Serikali Kwa kutambua mchango wa UTPC na Press Clubs nchini pamoja na taasisi nyingine za habari nchini katika maendeleo ya nchi.
Alisema Press Clubs na UTPC zipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha wananchi habari ambazo zitawasaidia kupata maendeleo.
Nsokolo pia alimuomba Msemaji mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa idara ya habari Maelezo kushughulikia changamoto zinazowakabili wanahabari nchini na hasa sheria, mikataba ya ajira na ujira, mambo ambayo ameahidi kiyashughulikia kupitia bodi ya ithibati itakayoundwa hivi karibuni.
Aidha Nsokolo amempongeza Msigwa Kwa ubunifu mbalimbali tangu ateuliwe kushika nyadhifa hizo, ubunifu ambao umefanya wananchi kupata taarifa za Serikali Kwa urahisi na waandishi kupata taarifa mbalimbali kupitia mikutano inayofanyika kila jumapili ya wiki.
Msemaji mkuu wa Serikali katika mkutano wake na waandishi wa habari pamoja na mambo mengine ametoa taarifa kuhusu maendeleo ya utoaji chanjo ya Uviko 19 na kuwataka wananchi kujitokeza kuchanja ili kujikinga na ugonjwa huo hatari.
 

 

Read More
Blog

MARA PRESS CLUB WAENDESHA MDAHALO

Mdahalo kuhusu Uhuru wa Kujieleza, Haki ya kupata taarifa na Maadili ya Uandishi wa Habari umemalizika leo mkoani Mara.
Mdahalo huu umeandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara (MRPC) chini ya ufadhili wa IMS na UTPC.
Mdahalo huu umejadili kuhusu umuhimu wa Uhuru wa Kijieleza na Haki ya kupata taarifa namna vinavyochangia kuwa na jamii yenye taarifa na inayoweza kufanya maamuzi sahihi.
Mbali na hilo, washiriki wameazimia mambo mengine mengi ikiwemo kuendelea kutoa maoni kwa ajili ya kuboresha sheria zinazominya uhuru wa habari nchini lakini pia kuwepo kwa chombo maalumu kitakacho tetea maslahi ya waandishi wa habari Tanzania.
Read More
Blog

UTPC KUANDAA KANUNI ZA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI

Mchakato wa kukusanya maoni kuhusu uandaaji wa kanuni za maadili ya uandishi wa habari wakiwemo watoa maudhui mtandaoni, umemalizika leo mkoani Mwanza kwa Mwanza Press Club kushiriki kama klabu ya mwisho kuandaa mkutano huu.
Tangu mchakato huu umeanza, klabu za waandishi wa habari 28 zimeshirikishwa kwenye mchakato huu kwa nyakati tofauti.
Klabu za Waandishi wa Habari ambazo zilipewa nafasi ya kuandaa mikutano hii na kutoa nafasi kwa klabu za jirani kutuma wawakilishi wao ni Dar es Salaam, Arusha, Zanzibar, Kigoma, Iringa, Dodoma, Mtwara na Mwanza.
Mikutano hii ni moja ya utekelezaji wa shughuli zilizopo kwenye mradi wa ushirikiano kati ya UTPC na IMS (International Media Support) ambao mradi huu umelenga kuzijengea uwezo taasisi za kihabari kushiriki katika ushawishi kuhusu uhuru wa habari na uhuru wa wananchi kupata taarifa.
Mradi huu unaendeshwa na shirika la International Media Support la nchini Denmark, ambao wamefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union).
Read More
Blog

MWANZA PRESS CLUB YAENDESHA MDAHALO

Mwanza Press Club leo imeendesha mdahalo kuhusu Maadili ya Uandishi wa habari, Uhuru wa Kujieleza na Haki ya kupata taaarifa, mdahalo ambao ulifunguliwa rasmi na Afisa Habari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Abel Ngapemba ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Mhandisi Robert Gabriel.
Mdahalo huu umejumuisha waandishi wa habari kutoka Klabu za Waandishi wa Habari za mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Simiyu.
Pamoja na ushiriki huo kutoka Press Clubs, pia Mdahalo huu ulijumuisha wadau muhimu wa habari kutoka ofisi ya Mkuu ya Mkoa wa Mwanza ambayo iliwakilishwa na Afisa Habari wake Bw. Abel Ngapemba, kutoka TCRA alikuwepo Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa Bw. Francis Mihayo, kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, iliwakilishwa na Inspector Mwita Robert na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Nyamagana (Mh. Stanslaus Mabula) iliwakilishwa na Bi. Florah Magabe.
Pamoja na kujadili mambo mengi kuhusu Maadili ya Uandishi wa Habari, Haki ya kupata taarifa na Uhuru wa Kujieleza, wajumbe wa mdahalo huu wamekubaliana kuendelea kufanya mambo makubwa matano kama maazimio ya Mdahalo huo.
1. Kuitisha Mkutano mkubwa wa wadau na waandishi wa habari kanda ya ziwa kujadili changamoto zinazoikabili tasnia ya habari na utatuzi wake. Mkutano huu utaitishwa kwa ushirikiano wa TCRA kanda ya ziwa, UTPC na MPC.
2. Kuandaa utaratibu wa kuendelea kujengeana uwezo kwa kutumia midahalo na mafunzo kwa ushirikiano wa waandishi na wadau wa habari kwenye maeneo mtambuka ambayo yanawakutanisha wadau na waandishi wa habari mara kwa mara.
3. Kuendelea kutoa maoni ya kuboresha sheria zinazogusa tasnia ya habari nchini, mfano EPOCA, MSA na Statistics Act
4. Kuimarisha mahusiano kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari hasa hasa taasisi za serikali kwa kutengeneza WhatsApp Group ili kuongeza wigo wa kupeana taarifa mara kwa mara.
5. Kufanya tafiti na kutoa machapisho yatakayoendelea kuongeza uelewa na kuhamisha masuala mazima ya Uhuru wa Kujieleza, Uhuru wa kutoa na kupata taarifa na maadili ya uandishi wa habari.
Mdahalo huu ni utekelezaji wa moja ya shughuli zilizomo kwenye mradi wa ushirikiano kati ya shirika la IMS (International Media Support) na UTPC.
Shughuli nyingine ni mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari, midahalo ya ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari, kuandaa kanuni za maadili ya uandishi wa habari na ufwatiliaji wa madhila kwenye tasnia ya habari.
Read More
Blog

WAFANYAKAZI WA UTPC WAJENGEWA UWEZO

Mafunzo ya ndani ya siku tatu kwa wafanyakazi wa UTPC ya namna bora ya kufanya Tathmini na Ufuatiliaji wa miradi (Monitoring and Evaluation) yamemalizika katika ofisi za UTPC.
Mafunzo haya yamewezeshwa na shirika la IMS ambalo UTPC inafanya nalo kazi kupitia mradi wa ushirikiano unaolenga kuzingea uwezo taasisi za kihabari nchini kushiriki kwenye ushawishi wa kuboresha uhuru wa habari, uhuru wa wananchi kupata taarifa na upatikanaji wa haki za msingi.
Mashirika mengine yanayotekeleza mradi huu na ambayo yamejengewa uwezo ni MISA TAN, TAMWA, MULIKA na ZANZIBAR YOUTH FORUM
Read More